MKUFUNZI WA MASWALA YA BIASHARA NA MASOKO REHEMA KASULE AWAPA ELIMU MANJANO DREAM MAKERS

00:04 Jason 0 Comments

Mkufunzi wa maswala ya biashara Mama Rehema Kasule kutoka nchini Uganda akiwapa elimu wanafunzi wa Manjano Foundation jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye majukumu yao ya kila siku ikiwemo kutengeneza uhusiano na watu waliofanikiwa kwa kuwa itasaidia kujifunza mengi.Pia namna ya kujiamini kuwaza mafanikio zaidi kuwa lazima wafanikiwe na kuachana kabisa na mawazo ya kushindwa akiwa sambamba na Afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions, Mama Shekha Nasser. 
Akieleza zaidi Mama Kasule amewataka Washiriki wa Manjano Dream Makers kama wanataka kufanikiwa kazi zao za upambaji na biashara zao ni lazima wafanye kwa moyo mmoja kutoka ndani ya nafsi pia kuachana na fikra za kukata tamaa na maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa. Kwa upande afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Manjano Foundation mama Shekha Nasser amewataka washiriki hao kuongeza juhudi pia kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliofundishwa katika mafunzo hayo.
Mama Rehmah Kasule alikuwa jijini Dar akihudhuria kwenye semina ya siku 4 ya #PSIPSE "Partnership to Strengthen Innovation and Practices in Secondary Education.
Baada ya semina yake, mama Kasule akajitolea siku moja kuja kutoa mafunzo kwa washiriki wa Manjano Dream Makers ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa washiriki walio wengi wa Vital Voices (na yeye akiwa mmojawapo) kwamba kila mwanamke ajitolee kuwasaidia au kuwafundisha wanawake vijana kitu anachokijua, yaani "Pay it Forward."

0 comments:

KARIBU UJUMUIKE NA WAZAZI WENZAKO KWENYE JUKWA LA KUJADILI MALEZI YENYE MALENGO

02:37 Jason 0 Comments

Ni ukweli usiopingika kuwa waazazi wote hupenda kuona watoto wao wakikua katika maadaili yanayopendeza na ikiwemo kufaulu vizuri katika masomo yao na hata wafikiapo umri wa kujitegemea wawe vijana wenye maono bora.
Hapo nyuma hakukuwa na mitaala ya kuweza kuwasaidia wazazi kukuza watoto vile inavyotakikana, hivyo ilipelekea watoto wengi kushindwa kufikia malengo yao na lawama walitupiwa wazazi wao.
Njoo ujiunge sasa na wazazi wenzako kwa mara ya kwanza Tanzania inakuletea (Malezi yenye malengo) ni jukwaa la majadiliano,maoni,na njia mbadala za kuwalea watoto wetu.
Nafasi ni chache jisajili mapema
Karibuni sana.
Wazungumzaji watakuwa Mrs Grace Makani Tarimo kutoka  Grace Inc Ltd na Dr. Elie Waminian (PHD) Kutoka Marekani

Namba ya simu 0754-461741

11/06/2016.
Hyatt Regency Hotel

0 comments:

SHEAR ILLUSIONS AFRICA YAADHIMISHA MWAKA MMOJA TANGU UZINDUZI WA KIPODOZI CHA LUV TOUCH MANJANO

23:21 Jason 0 Comments

Kampuni ya Shear Illusions imehadhimsha mwaka mmoja tangu uzinduzi wa Kipodozi Pendwa cha LuvTouch Manjano. Kipodozi cha LuvTouch kilizinduliwa mnamo tarehe 31 May mwaka 2015 jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi aliyekuwa mke wa Waziri Mkuu wa zamani Mh. Mama Tunu Pinda katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Katika maadhimisho hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions mama Shekha Nasser amewashukuru wanawake  na Watanzania kwa ujumla kwa kufanikisha kutambulika kwa bidhaa za LuvTouch Manjano. LuvTouch ni Brand ya Kipodozi cha kwanza nchini inayomilikiwa na mwanamke mzalendo wa Kitanzania. Kupitia bidhaa hiyo pia imeanzisha Taasisi ijulikanayo kama 'Manjano Foundation' yenye lengo kuu ya kuwasaidia wanawake kiuchumi. Katika  mwaka mmoja tangu uzinduzi wa bidhaa za LuvTouch Manjano, Taasisi hiyo imefanikiwa kuwaelimisha zaidi ya wanawake 195 katika mikoa mitano nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Arusha na Dodoma. 

Pia katika kipindi cha mwaka mmoja wameweza kuwakopesha wanawake mitaji ya vipodozi vya LuvTouch Manjano yenye thamani ya shilingi milioni 45 (TSh.45,000,000). Akieleza zaidi mama Shekha Nasser amesema ataendelea kuwashika mkono wanawake wenzake kadiri ya uwezo wake unavyoruhusu kwa lengo la kumkomboa mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa Ajira.Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na wanawake walio washiriki wa mradi wa Manjano Dream-Makers na wadau (Mentors), washauri na watu waliojitolea kuwasaidia washiriki hao. 

Wanawake na washauri waliohudhuria hafla hiyo walimpongeza mama Shekha Nasser kwa moyo wake wa kujitolea na kuwabeba wanawake vijana. Mmoja wa wazungumzaji na mdau wa mradi, mwanasaikolojia maarufu aunt Sadaka Gandi alisema, ameishi na wanawake wengi nchini lakini hajawahi kuona Mwanamke mwenye moyo wa kujitolea kama wa Shekha. Amewaasa wanawake walionufaika na mradi huo kufanya kazi kwa bidii kupitia Mradi huo kwa kuwa wao wanabahati sana kunufaika kwa kuwa wapo wanawake wengi nchini wasiokua na kazi na wangetamani kunufaika lakini wamekosa nafasi hiyo

0 comments: