TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAENDELEA KUWANUFAISHA WANAWAKE
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa kutumia Vipodozi wakiwa kwenye mafunzo kwa njia ya Vitendo..Wanawake wachache wa jiji la Dar es salaam wameendelea kunufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Washiriki hawa wameendelea kufundishwa matumizi sahihi na ueledi wa kutumia vipodozi (makeup) mbalimbali kutokana na nyakati tofauti. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na mtaalamu wa mambo ya urembo na muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation mama Shekha Nasser. Mafunzo haya yenye lengo la kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukossefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo
Mafunzo haya yamegawanywa katika awamu mbili ili kumsaidia mjasiriamali wa kike kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake
Awamu ya Pili mshiriki anafundishwa Matumizi sahihi ya Vipodozi kuendana na wakati, mfano office makeup, day, evening na namna ya kumpamba bi Harusi. Pia wanafundishwa namna bora ya kutumia Vipodozi vya LuvTouch Manjano kwa lengo ya kuwa kila mshiriki atakayehitimu mafunzo haya aweze kujiajiri na kujitegemea kwa kuendesha maisha yake ya kila siku kwa kuwapambamba watu wenye Shuguli Mbalimbali kama vile fashion, sendoff, harusi nakadhalika
Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa (paired) na Mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii watakaowaita 'Mentor'. Mentor night kama dada wa kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima.
Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea
0 comments: