MKUTANO WA WADAU WA MRADI WA MANJANO DREAM MAKERS
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa Mama Shekha Nasser Akieleza Jambo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Mradi wa Manjano Dream Makes akiwa Pamoja na Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila.
Lengo la Mkutano huo ilikuwa ni kuwakutanisha Dream Makers Pamoja Mantor's Wao ,Uongozi Na Wafanyakazi wa Manjano Foundation na Mkufunzi wa Maswala ya Biashara kwa lengo la kutadhimini Maendeleo ya Mradi huo Tangu Ulipoanzishwa Pamoja na Changamoto Mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa Kutekeleza Mradi Huo.
Manjano Drem Makers ni Mradi ulioanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali.Mafunzo Chini ya Taasisi ya Manjano Foundation.Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.
Mpaka sasa zaidi ya wanawake 25 Kutoka Mkoa wa Dar es salaam wamenufaika na Mafunzo ya Ujasiriamali ya Namna ya Kuendesha Biashara zao na wamewezeshawa Mitaji ya Kuanzisha Biashara zao kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano.
Washiriki wa Mradi wa ujasiriamali kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mwanamitindo Flaviana Matata. Mkurugenzi wa 8020 Fashion Shamim Mwasha akiwa katika Picha na baadhi ya wanufaika wa Mradi wa kuwewezesha wanawake kuwa wajasiriamali kupitia vipodozi vya Luv Touch Manjano ulio chini ya Taasisi ya Manjano Foundation
Picha ya Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa Mama Shekha Nasser ( Wa pili kulia) Akiwa na Mentor's wa Manjano Foundation ambao ni washauri wakuu wa Wanawake walionufaika na Mradi wa Ujasiriamali kupitia Vipodozi vya Luv Touch Manjano.
Picha ya Pamoja Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamali yaliochini ya Taasisi ya Manjano foundation wakiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions afrika Mama Shekha Nasser (Watatu kutoka kulia waliokaa),Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Felix Maganjila (wa Pili kulia waliokaa), Meneja mradu huo Mama Franswaz Msinga (Wapili kutoka Kushoto waliokaa) Pamoja na washauri wakuu wa wanawake walionufaika ma Mradi Huo.
0 comments: