NAIBU SPIKA WA BARAZA LA WAKILISHI ZANZIBAR AKUTANA VITAL VOICES GROW MJINI UNGUJA

01:04 Jason 0 Comments

Image may contain: 1 person, sitting 
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma  Akizungumza na Wanawake wa Kikundi cha Vital Voices Grow Kutoka Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika Mjini Unguja.
Kikundi cha Vital Voices Grow (VVGrow) kutoka Afrika Kusini  mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa) kwa mwaka 2015/2016  kimemtembelea Mheshimiwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma katika ofisi zake mjini Unguja, Zanzibar.
Kikundi hicho kilichokuwa na ujumbe wa watu sita wakiongozwa  na mwenyeji wao Bi.  Shekha Nasser ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Shear Illusions na muasisi wa vipodozi vya Manjano walipata fursa ya kumtembelea Naibu Spika kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Wanakikundi hao.
Mheshimiwa Bi. Mgeni ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Unaibu Spika katika historia ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Katika ziara hiyo, VVGrow pia walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo wanawake na maendeleo ya kiuchumi kutoka kwa Bi. Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge Zanzibar (UWAWAZA). Pia ilikuwa ni fursa kwao kuonesha heshima yao kwa viongozi wa wanawake ambao wanaboresha ulimwengu na kuhamasisha usawa.
Kikundi cha VVGrow kiko mjini Zanzibar  kwa lengo la kujumuika na pia kutathmini na kujadili mawazo ambayo yatawasaidia kukua kwa wanakikundi wao binafsi na pia kukuza  biashara zao kwa kujenga ajira na kukuza uchumi.
VV GROW Fellowship ni fursa kwa wanawake ulimwenguni wenye ushindani mkubwa wa mafunzo ya mwaka mmoja wenye lengo la kusaidia wanawake wamiliki wa biashara ndogo ndogo na za kati katika mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Afrika kusini mwa Sahara.

0 comments: