UZINDUZI WA MAFUNZO YA KUJENGA AJIRA KUPITIA VIPODOZI KWA WANAWAKE JIJINI MBEYA WAFANA
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akizungumza wakati Akifungua Mafunzo ya Ujasiriamali Mkoa wa Mbeya
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede kawataka wanawake wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema leo jijini Mbeya alipokuwa akifungua mafunzo ya wanawake 30 juu ya masuala ya ujasiriamali na urembo yanayoendeshwa ta Taasisi ya Manjano Foundation .
“Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kwa kutumia bidhaa ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake wadogo kupata mafunzo ili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema meneja wa SIDO.
Mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser Akizungumza Machache kwenye ufunguzo huo.
Ameongeza kuwa mbali na Taasisi ya Manjano Foundation kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe kuwaunganisha wanawake hao na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ili kupata mitaji ya kuanzisha biashara zao.
Mgeni Rasmi akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamamli Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.
0 comments: