TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MKOANI DODODMA
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dodoma.
Awamu ya Saba na ya mwisho katika budget ya Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 150 kutoka mikoa Mitano Tanzania yamemalizika Mkoani Dodoma. Wanawake 30 wa mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa wanawake hao 150 walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yamefanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Arusha na kuhitimisha na Mkoa wa Dodoma.
Pamoja na mafunzo, kila mshiriki anaunganishwa na mwanamke mmoja mwenye mafanikio katika biashara au uongozi katika jamii kwa lengo la kumuongoza katika safari yake ya biashara kwa muda wa mwaka mzima. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wanawake wa mji wa Dodoma walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani.
Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.
0 comments: