TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAENDELEA KUWAELIMISHA WANAWAKE KUTOKA ARUSHA NA KILIMANJARO
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhyGwKQnXLt-WFP8TESBWSQznW1DW1wKr28ZH2B6kcrVEOfpK0Ick4slN44Yde5G75w2KuY_wWJQm1DH7ns6R_x59UuNwr8JUS5TqSD6xFTUCv71iMtwzg8olRp_noRCEUck_7Q1BMEdWI/s640/12715590_10153396450380905_2505122448421189644_n.jpg)
Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa arusha yameingia awamu ya pili.Washiriki wamepata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu vipodozi vya LuvTouch Manjano na namna ya kuvitumia. Mkufunzi na Mkurugenzi wa taasisi ya Manjano Foundation amependekeza wanawake wa jiji la Arusha kutumia vipodozi kwa usahihi kwa lengo la kujijengea heshima na kujiongezea kipato katika kazi yao ya upambaji.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation na Mkufunzi wa Maswala ya Vipodozi Mama Shekha Nasser Akitoa elimu Kuhusu Matumizi Sahihi ya Vipodozi Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Jiji la Arusha
Akielezea zaidi alisema matumizi sahihi ya vipodozi hasa vya LuvTouch Manjano vitakupa kazi nzuri na bora ambayo kila mteja ataipenda na kulifanya soko la kila mwanamke kukua kutokana na ubora wa kazi ya mikono yake
0 comments: