Wanawake wa jiji la Mwanza wamshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions
Wanawake wa jiji la mwanza walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali wamemshukuru afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na mkurugenzi wa taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Mwanza.
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake. Pia wanawake hao watanufaika na mikopo ya bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano kwajili ya mitaji ya kuanzisha biashara ya kupamba maharusi na kuuza vipodozi
0 comments: