MRADI MANJANO DREAM MAKERS WA KUKWAWEZESHA MANAWAKE WAJASIRIAMALI WAINGIA ZANZIBAR
Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba kwajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 759413234
0 comments: