MAMA SHEKHA NASSER ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA NA WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA JIJI LA DAR ES SALAAM
Mama Shekha Nasser Akikata Keki ikiwa ni kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.
Mama Shekha Nasser aliamua kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula mlo wa jioni pamoja na wafanyakazi wake wote wakiwa na washiriki wa Manjano Dream-makers. Ikiwa ni utamaduni wa kampuni yake kufanya sherehe ya kuuaga mwaka alitumia kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa pamoja na wanawake Wajasiriamali wa Taasisi yake aliyoianzisha ya Manjano Foundation ambayo amewawezesha kwa kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na pia kuwafundisha ulimbwende pamoja na kuwakopesha mitaji ya bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano kufanya Biashara hasa kwa Kutumia Vipodozi hivyo pendwa Tanzania. Mama Shekha amewashukuru sana na amewaasa wanawake hao kupambana zaidi kila kukicha kwa lengo la kila mwanamke kufikia malengo aliyojiwekea kuwa mfanyabiashara wa kujitegemea.
Mama Shekha Nasser akipokea zawadi mbalimbali alizotunzwa na wanawake wajasiriamali wa Manjano Dream-makers na waajiriwa wa kampuni ya Shear illusions. Wanawake wajasiriamali walimshukuru sana Mama shekha kwa moyo wake wa kujitolea ambapo amewawezesha kupiga hatua kwa kugusa maisha yao ya kila siku na pia kuwakutanisha na watu wengi wakiwemo wateja wao na mentors. Wafanyakazi pia walishukuru na kusema walifurahi kutolewa dinner na boss wao na kufurahia chakula cha jioni na Mama yao kwa kuwa mara nyingi wanaonana mazingira ya kazi tu
Mama Skekha Nassea Katika Picha ya Pamoja na wateja waliomtembelea Kupata Huduma Mbalimbali .
0 comments: