MWANASAIKOLOJIA ANTI SADAKA AWAFUNDA WANAWAKE WA JIJI LA MWANZA

23:16 JAFE MALIBENEKE 0 Comments

Mwanasaikolojia Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mwanza yanayoendesha na  Taasisi ya Manjano foundation yanaoendelea kwenye ukumbi wa Rocky city Jijini Mwanza.
Mwanasaikolojia Anti Sadaka amewafunda wanawake wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo ya ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa  na wataalamu kutoka taasisi ya Manjano  Foundation  yanayoendelea Jijini Mwanza kwa wiki nzima. Anti Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake hao kujitambua wao ni nani  wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la kufikia malengo yao.
Wanawake wa Mkoa wa Mwanza wakifuatilia kwa amkini Mada zilizokuwa zinaendeshwa   kwenye Mafunzo hayo.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mkoani Mwanza kuchangamkia FURSA zinazowazunguka mapema iwezekanavyo. Alisisitiza umuhimu wa usafi wao binafsi na mazingira yao ya kazi kupewa kipao mbele kwa sababu usafi humlinda mteja asipate breakout ya ngozi yake na kuridhika na huduma yake yaani "Smart You & Environment."
Semina hiyo inawanufaisha wanawake wa Mwanza kwa lengo la kuwaongezea kipato na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira. Baada ya washiriki kupata mafunzo ya biashara na urembo watapatiwa  MIKOPO kutoka Taasisi ya Manjano  Foundation  kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Mwanasaikolojia Anti Sadaka Akiwa katika Picha ya Pamoja na wanawake wa Mkoa wa Mwanza waliojitokeza  kwenye Mafunzo ya Ujasiriamali  yanayoendeshwa  na Taasisi ya Manjano Foundation.
Washiriki wa mafunzo hayo  wameushukuru uongozi wa Taasisi ya Manjano  Foundation kwa kuwakumbuka na kuwaletea Mradi huo jijini Mwanza. Wakieleza zaidi wamesema kwa muda mrefu wamekuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu matumizi sahihi ya vipodozi lakini walikosa elimu hiyo ya kuwa Makeup Artists.

0 comments: