MAHAFALI YA PILI YA CHUO CHA MANJANO BEAUTY ACADEMY YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Wahitimu wa Chuo cha Urembo cha Manjano wametunikiwa vyeti katika nyanja ya urembo na vipodozi (Cosmetology). Baadhi ya wahitimu waliofika kwenye mahafali hayo walivikwa taji kama ishara ya mafanikio ya kitaaluma, na kuweka alama kwenye hatua muhimu katika maendeleo yao ya kitaaluma kwenye tasnia ya urembo na vipodozi. Zaidi ya wanafunzi 87 wamehitimu kwa mwaka huu wa 2018 na wataendelea na mafunzo ya utarajali (internship program) kwa kipindi cha miezi 12 katika masalon, kampuni na taasisi mbalimbali zenye kujihusisha na urembo na vipodozi ili kuweza kujijengea ujuzi (skills) na uzoefu (experience) katika kazi zao. Sherehe ilizinduliwa na Mkufunzi kutoka VETA, Mwl. Salehe Omari, akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam, mama Florence Kapinga. 
Mkuu wa Chuo cha Urembo mama Shekha Nasser akizungumza machache wakati wa mahafali ya pili ya Chuo cha Manjano Beauty Academy. Amewataka wanawake kujiongezea elimu ya matumizi sahihi ya Vipodozi na Urembo ili kuweza kutoa huduma sahihi na yenye ueledi kwa wananchi. Mama Shekha alisema Tanzania kuna upungufu mkubwa wa Wataalamu, hasa walimu wenye sifa za kufundisha elimu ya Urembo na Vipodozi, hivyo aliwashauri wanawake wengi kujiunga na Chuo cha Manjano Beauty Academy ili waendeleze tasnia hii na kuboresha huduma zao kwa wateja. Aidha alitaja changamoto kubwa alizokabiliana nazo wakati anaanzishi Chuo hicho ikiwemo ukosefu wa wataalamu wazawa wa maswala ya Urembo na Vipodozi. Akieleza zaidi alisema sekta ya urembo ina fursa kubwa kwa ajira na inaweza kusaidia kujiongezea kipato na kuondokana na ukosefu wa ajira na umasikini.
Mgeni rasmi, uongozi wa Chuo cha Manjano Bauty Academy na Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni rasmi, Mwl. Salehe Omari, naye pia aliwashukuru wanawake wa Kitanzania waliojiunga kwenye chuo hicho kwa lengo la kupata ujuzi wa maswala ya urembo na vipodozi. Alisema Urembo, Vipodozi na mitindo ni moja kati ya sekta zinazoajiri mamilioni ya wanawake kwa sasa, na kuchangia kwa kiasi kwenye pato la Taifa. Akiendelea zaidi alisema, elimu na mafunzo kwa vitendo (Vocational training) ni elimu na mafunzo ambayo yanayotoa ujuzi na elimu muhimu kwa ajili ya ajira. Elimu ya aina hii ni ambayo humuandaa mtu kufanya kazi katika fani mbalimbali, kama biashara, utengenezaji wa vitu, au kama fundi. Hivyo aliwausia wahitimu kuitumia vizuri elimu na ujuzi walioupata kwenye Chuo cha Manjano. Alielezea pia kwa kusema elimu ya ufundi na ujuzi ni muhimu katika kuleta usawa kwenye jamii kwani ni moja ya kitovu cha kuleta maendeleo na kuendana na kasi ya Awamu ya Tano ya Uchumi wa Viwanda. Elimu ya ufundi, stadi za kazi au wa kazi za mikono ni mojawapo ya vipaumbele vya UNESCO. Kwani elimu hii inasaidia kuendeleza elimu ya ubora na usawa na fursa za kujifunza kwa wakati wote ule haijalishi umri wako, “wewe ni mwanafunzi wa kudumu alisema.”
Tunawatakia wasomi wetu wote kila la kheri katika kazi zao. Mkuu wa Chuo cha Urembo Mama Shekha Nasser akizungumza.
Shekha ni mmiliki wa kampuni ya Shear Illusions na mnamo mwaka 2015, kupitia bidhaa za LuvTouch Manjano alianzisha chuo cha Manjano Beauty Academy kwa lengo la kutoa elimu na ujuzi wa kuwawezesha wasichana na wanawake kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia tasnia ya Urembo na Vipodozi.



TAASISI YA MANJANO FOUNDATION YATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA KIGOMA

Mradi wa Kuwawezesha vijana wa kike na wanawake kiuchumi kupitia Tasnia ya Urembo na Vipodozi ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wamemaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma Yaliofanyika kwa wiki mbili kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yaliyotolewa bure yamewanufainsa wanawake 20 kutoka Mkoani Kigoma na vitongoji vya jirani. 

 Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. Awamu ya pili walipata ujuzi jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi salama vya LuvTouch Manjano.


 Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba ili waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara zao wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea. Taasisi ya Manjano imefanikiwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 500 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Unguja - Zanzibar

. Wengi wa wahitimu wa mradi wa Manjano Dream-Makers wamefanikiwa kuanzisha biashara zao na kuwa mawakala wa bidhaa za LuvTouch Manjano. Kwa mwaka huu taasisi ya Manjano wanajipanga pIa kumalizia kwa kuwawezesha kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wa kike na wanawake wa Mkoa wa Tabora..

CHAMA CHA WATAALAMU WA UREMBO NA VIPODOZI TANZANIA (CWUVT) CHAANZISHWA KUENDANA NA SERA ZA AWAMU YA TANO

Chama cha Wataalam wa Urembo na Vipodozi Tanzania (CWUVT) wakutana Jijini Dar es salam kwa lengo la kuwakutanisha  pamoja wataalamu wa ngozi, wataalamu wa urembo, wataalam wa saluni,  wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi. Wanachama waasisi wa chama hicho walikutana chini ya Mwenyekiti Mama Shekha Nasser. Dhira ya Asasi hiyo ni kuinua, kuunganisha na kutumikia sekta ya Urembo na Vipodozi, watabibu wa ngozi na wataalamu wa Saluni ambao huboresha maisha ya watu kila siku. Pia kujenga na kudumisha wanachama ambao uwepo wao ni kukuza na kuunga mkono utaalam katika tasnia ya Urembo na Vipodozi kwa ujumla wake. 

Wajumbe waasisi walioudhuria mkutano huo wameipitisha Katiba ya Chama hicho na kuazimia kujitoa na kushirikiana kwa pamoja katika kuelimisha, kuhudumia na kutetea haki za wataalam wa saluni, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa za vipodozi katika tasnia ya Urembo na Vipodozi. 

Chama hicho kimeona jinsi tasnia hii inakua kwa kasi, na mabadiliko ya kitechnologia hivyo wameona ni muda muafaka kwa Watanzania kuwa na uelewa zaidi kuhusu tasnia hiyo kubwa yenye Fursa kubwa ya Ajira hapa Nchini na kuchangia katika kukua kwa uchumi wa nchi na hata kuingiza mapato ya kigeni.

NAIBU SPIKA WA BARAZA LA WAKILISHI ZANZIBAR AKUTANA VITAL VOICES GROW MJINI UNGUJA

Image may contain: 1 person, sitting 
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma  Akizungumza na Wanawake wa Kikundi cha Vital Voices Grow Kutoka Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika Mjini Unguja.
Kikundi cha Vital Voices Grow (VVGrow) kutoka Afrika Kusini  mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa) kwa mwaka 2015/2016  kimemtembelea Mheshimiwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma katika ofisi zake mjini Unguja, Zanzibar.
Kikundi hicho kilichokuwa na ujumbe wa watu sita wakiongozwa  na mwenyeji wao Bi.  Shekha Nasser ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Shear Illusions na muasisi wa vipodozi vya Manjano walipata fursa ya kumtembelea Naibu Spika kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Wanakikundi hao.
Mheshimiwa Bi. Mgeni ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Unaibu Spika katika historia ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Katika ziara hiyo, VVGrow pia walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo wanawake na maendeleo ya kiuchumi kutoka kwa Bi. Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge Zanzibar (UWAWAZA). Pia ilikuwa ni fursa kwao kuonesha heshima yao kwa viongozi wa wanawake ambao wanaboresha ulimwengu na kuhamasisha usawa.
Kikundi cha VVGrow kiko mjini Zanzibar  kwa lengo la kujumuika na pia kutathmini na kujadili mawazo ambayo yatawasaidia kukua kwa wanakikundi wao binafsi na pia kukuza  biashara zao kwa kujenga ajira na kukuza uchumi.
VV GROW Fellowship ni fursa kwa wanawake ulimwenguni wenye ushindani mkubwa wa mafunzo ya mwaka mmoja wenye lengo la kusaidia wanawake wamiliki wa biashara ndogo ndogo na za kati katika mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Afrika kusini mwa Sahara.

MENEJA WA SIDO MKOA WA MTWARA AZINDUA RASMI MAFUNZO YA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI CHINI YA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION


 Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa Akizungumza Machache wakati Akizindua Rasmi mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa Mtwara akiwa wa Wawezeshaji kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa kawataka wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema mkoani Mtwara alipokuwa akifungua mafunzo hayo kwa wanawake wajasiriamali katika sekta ya vipodozi na urembo. Mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wanawake 30 waliotuma maombi na kuchaguliwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza zaidi amesema “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia bidhaa hizo” 
Baada ya kuhitimu mafunzo haya washiriki hao wataunganishwa na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ya kupata mitaji ya kuanzisha bishara
Mwezeshaji Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation Bi Ester Lukindo Akizungumza Machache wakati wa Uzinduzi Huo .
Bi Ester Lukindo aliyesoma hotuba kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama “Shekha Nasser alisema kuwa "wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo."
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi Mtwara ukiwa ni mkoa wa tatu tayari kufikiwa.

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUWAWEZESHA WANAWAKE WA MTWARA KIUCHUMI

Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuanzia Jumatatu, tarehe 27 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Mtwara. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Mtwara. 
Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mtwara wanafikia malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 25 Machi 2017 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mtwara.
Mafunzo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
Awamu ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 784 661 080 au +255 714 646 322



UZINDUZI WA MAFUNZO YA KUJENGA AJIRA KUPITIA VIPODOZI KWA WANAWAKE JIJINI MBEYA WAFANA

 Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akizungumza wakati Akifungua Mafunzo ya  Ujasiriamali  Mkoa wa Mbeya 
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede kawataka wanawake wa Mkoa wa Mbeya  kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema leo jijini Mbeya  alipokuwa akifungua mafunzo ya wanawake 30 juu ya masuala ya ujasiriamali na  urembo yanayoendeshwa ta Taasisi ya Manjano Foundation .

 Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akiwa Ameambatana na Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Mama Fatuma Kange Pamoja na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser
 “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kwa kutumia  bidhaa ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake wadogo kupata mafunzo ili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema meneja wa SIDO.
 Mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser Akizungumza Machache kwenye ufunguzo huo.

Ameongeza kuwa mbali na Taasisi ya Manjano Foundation kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe kuwaunganisha wanawake hao na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ili kupata mitaji ya kuanzisha biashara zao.

Mgeni Rasmi akiwa katika Picha ya Pamoja  na Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamamli Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.